Liverpool inajiandaa kumuuza mshambuliaji wale Mbrazili Roberto Firmino kwenda Barcelona kwa dau la Paundi Mil 16 sawa na Tsh Bil. 50. 5 katika majira ya kiangazi
Kocha Jurgen Klopp anaweza kumwachia Firmino kutoka na na kiwango anachokionyesha Diego Jota, ambaye tangu atue klabuni hapo amekuwa chaguo namba moja.
Kwa sasa Firmino ndiye alipewa majukumu ya kuongoza mashambulizi kwa sababu ya kukosekana kwa Mohamed Salah na Sadio Mane ambao wapo kwenye michuano ya Afcon, inayoendelea Cameroon
0 Maoni