Uongozi wa Mabingwa wa Ulaya, Chelsea unatarajia kumpiga faini Straika  wao Romelu Lukaku baada ya mchezaji huyo kufanya mahojiano yake na kituo cha Sky Sport Italia .



Licha ya kuomba radhi Kwa uongozi wa klabu hiyo mchezaji huyo imetajwa anaweza kupigwa faini ya £500,000 sawa na Billion 1.2 Pesa za Kitanzania .





Lukaku aliondolewa kwenye kikosi kilichovaana  Liverpool na sasa anategemewa kurejea kikosini Kwenye Mchezo wa Nusu fainali ya Carabao Cup dhidi ya Tottenahm Hostpurs Leo .



"Nmeomba radhi kwa manager, uongozi na wachezaji wenzangu,Lakini pia nichukue fursa hii kuwaomba radhi mashabiki wa Chelsea haikuwa jambo zuri mimi kutamka vile.



Tunahitaji kusonga mbele na niahidi ushindi kufanya vizuri kwenye michezo inayofuata"amesema Lukaku.