Mshambuliaji  wa Namungo Fc Reliants Lusajo amechagulia kuwa  Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya NBC mwezi Disemba, 2021.

 




Kikao cha kamati ya Tuzo za TFF kimemchagua Lusajo  baada ya kuonesha kiwango kizuri  kwa mwezi Desemba  akifunga mabao matatu kwa timu yake na kuchangia  mafanikio klwa Namungo ikipanda kutoka nafasi ya 13 hadi ya 8 katika msimamo wa ligi kuu.