Manchester City imeendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kuu England, baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0  dhidi ya mabingwa wa ulaya, Chelsea mchezo uliochezwa katika dimba la Ettihad, Manchester.

 



 

Bao pekee kwenye mchezo huo limefungwa Kevin De Bruyne dakika ya 70, ambao kwa sehemu kubwa ulitawaliwa na wenyeji Man City.

 

Pep Guardiola anaonekana kuwa amedhamiria kutwaa ubingwa msimu akiongoza msimamo na alama 56 akiicha Chelsea na alama 43 katika nafasi ya pili.