Manchester United imeendelea kusususa kwenye ligi kuu ya
England baada ya jana usiku kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na Aston Villa
mchezo uliopigwa katika dimba la Villa Park.
Hadi Dakika ya 67 United ilikuwa inaongoza kwa mbao 2-0
magoli yaliofungwa na Mreno Bruno Fernandes dakika ya 6’ na 67’
Mabadiliko yaliofanywa na kocha Stven Gerrard ya kumuingiza
Phillipe Countinho yalionaekana kuzaa matunda baada ya Jacob Ramsey kupacjhik
goli dakika ya 77.
Akicheza mechi yake ya kwanza kwenye uzi wa Villa Countinho,
akafunga goli la pili na kuisaidia villa kupata alama moja muhimu.
Kwa matokeo haya United kwenye msimamo wa Epl inashika nafasi 7 wakiwa na alama 32, wakati Villa ipo nafasi ya
13 na alama 23.
0 Maoni