Manchester United ipo mbioni kuisaka saini Mreno Ruben Neves
wa Wolverhampton Wanderers kwenye dirisha
hili dogo ili kuimarisha safu yao ya kiungo.
United wapo tayari kutoa Pauni Mil. 35 lakini Wolves wanahitaji kiasi cha pauni 40
ili wamwachie mchezaji huyo.
Neves 24, amebakisha mkataba wa miaka miwili ndani Molineux ana ndoto za kucheza michuano ya ligi ya
mabingwa ulaya, United wanataka kutumia michuano hiyo ya (uefa) kama chambo kumshawishi
kujiunga na Man Utd.
0 Maoni