Manchester United jana usiku Januari 19, imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Brentford kwenye mchezo wa ligi kuu ya England uliochezwa jana usiku.
Magoli ya United yamefungwa na kinda Antony Elanga dakika ya
55’ ambaye amepachika goli lake la
kwanza kwenye Epl, united wakaongeza bao la pili kupitia kwa Mason Greenwood dakika
ya 62’ akimalizia pasi safi ya Bruno
Fernandes.
Marcus Rashford akitokea benchi aliipa Man United goli la la
tatu dakika ya 77’ pasi nyingine ya Fernandes na kuihakikikishia kuondoka na alama tatu
Goli la Brentford limefungwa na Ivany Toney, United bado upo
nafasi ya Saba na alama 35
0 Maoni