Manchester United
imejitoa kwenye kinyang’anyiro cha kumsajili Erling Haaland baada ya nyota
kuripotiwa kupendelea kutua Real Madrid.
Haaland
anavutiwa na Meneja mpya wa Man United Rafl Rangnick lakini matarajio ya klabu
hiyo ambayo ipo kwenye kipindi cha mpito pamoja na kuwa hatarini kukosa UEFA
msimu ujao kunazima ndoto za kujiunga nayo.
Man United
inasaka fowadi hatari wa kucheka na nyavu atakayerithi mikoba ya Edson Cavani
ambaye huenda akaondoka kwenye timu hiyo majira ya kiangazi.
0 Maoni