Mshambuliaji wa Manchester United   Anthony Martial amekanusha madai ya Kocha Mkuu Ralf Rangnick kwamba hakutaka kuwa sehemu ya kikosi kilichotoka sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Aston Villa.

 

 


Martial anataka kuondoka ndani ya Manchester United na timu inayotajwa kuisaka saini yake ni Sevilla ambayo inahitaji kupata huduma yake.

 

Katika Uwanja wa Villa Park, United ilikuwa na wachezaji nane benchi kisha baadaye Rangnick aliweka wazi kuwa Martial hakutaka kuwa sehemu ya kikosi.

 

 

“Hakutaka kuwa sehemu ya kikosi, kwa kawaida angekuwepo lakini hakutaka hiyo ni sababu ambayo hakusafiri nasi,”.

 

 

Tangu kuwasili kwa Rangnick bado mambo hayajakaa sawia tofauti na matarijio ya mashabiki wengi licha ya kikosi hicho kusheheni nyota wengi wakiongozwa na Cristiano Ronaldo.