Klabu ya Sevilla ya Hispania imefikia makubaliano ya kumsajili kwa mkopo  mpaka mwisho wa msimu winga wa Manchester United na timu ya taifa ya Ufaransa Antony Martial.



Nyota huyo amekosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha United na amekuwa akishinikiza kuondoka ndani ya Old Trafford.



Sevilla wamekubali kulipa mshahara wote wa mchezaji huyo hadi mwezi juni na atasafiri leo kuelekea Hispania kukamilisha taratibu za kujiunga timu.



Martial  amevutiwa zaidi na dili la kujiunga na Sevilla licha ya ofa kutoka kwa vibibi vizee vya Turin Juventus na Barcelona akiimini kujiunga na mabingwa hao  mara sita  wa ligi ya Europa ni sehemu sahihi na atapata nafasi ya kucheza.