Wachezaji wa Yanga Khalid
Aucho, Yanick Bangala, Djuma Shabani na Mukoko Tonombe, watakuwa sehemu ya kikosi cha hicho katika mchezo unaofuata wa nusu fainali ya
Kombe la mapinduzi dhidi ya Azam FC.
Yanga imetinga hatua hiyo mara baada ya kumaliza
vinara wa Kundi B kwa kukusanya pointi nne na kesho Jumatatu itacheza dhidi ya
Azam FC.
Kiungo Said Ntibazonkiza tayari
amewasili Zanzibar kwa ajili ya kuongeza nguvu na Yanick Bangala, Djuma Shabani
na Mukoko Tonombe tayari wameshamaliza mechi yao ya timu ya taifa Januari 6,hivyo wapo tayari hivyo huenda wakawa sehemu ya kikosi kitachocheza mchezo huo.
0 Maoni