Dakika 90, za mchezo wa  Azam Sports Fefederation Cup (ASFC) hatua ya 32 umekamilika, kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbao Fc, mchezo ulichezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.



Bao pekee la Yanga limefungwa na Mshambuliaji Fiston Mayele dakika ya 54, Yanga imesonga mbele kwenye michuano hiyo na kutinga hatua ya 16 bora.