Staa wa Ufaransa na PSG Kylian Mbappé amefikia makubaliano na
Real Madrid ya kusaini mkataba kama mchezaji huru ifikapo majira ya kiangazi,
kwa mujibu ripoti kutoka Ujerumani
Hii ni habari mbaya kwa PSG ambao walikataa ofa ya Paundi 154
mil, kutoka kwa Real Madrid kwenye majira ya kiangza mwaka jana
Mabingwa hao wa Ligue 1 walikataa ofa hiyo wakiwa na matumaini
ya kumshawishi mshindi huyo wa kombe la Dunia, kusalia Paris lakini inaonekana
dili hilo kukwama baada ya Mbappe kugoma kuongeza mkataba mpya.
0 Maoni