Beki wa kulia wa Paris Saint-Germain, Achraf Hakim jana
usiku, ameipeleka Morocco hatua ya robo fainali ya Afcon baada ya kufunga goli
la ushindi dhidi ya Malawi akifunga kwa faulo matata.
Free kick hiyo imemfanya staa mwenzake wa PSG Kylian
Mbappé kuandika kupitia ukurasa wake wa
Twitter kuwa Hakim ndiye beki bora wa kulia duniani.
Kwenye mchezo huo Malawi walikuwa wa kwanza kufunga
kupitia Gabadinho Mhango dakika ya 7’ na goli la kusawazisha kwa Morocco
likiwekwa wavuni na Youssef En- Nesyri dakika ya 45.
Morroco imetinga hatua kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Malawi
ambao wameingia hatua ya 16 bora kama (best
loser).
0 Maoni