Watu sita wameripotiwa kufariki na wengine 40 Wa kujeruhiwa katika msongamano uliotokea nje ya uwanja wa Paul Biya mechi ya hatua ya mtoano (16 bora) Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Cmeroon dhidi ya Comoro uliochezwa jana usiku Januari 24.
Picha za video zimeonesha mashabiki waking'ang'ana
kuingia kwa nguvu katika uwanja Paul Biya uliopo katika Mji Mkuu Yaounde.
Uwanja huo una uwezo wa kuwapokea watu 60,000,
lakini kwasababu ya masharti ya kuzuwia maambukizi ya Covid ulipaswa kupokea
80% pekee ya watu hao.
Maafisa wa mechi waliripotiwa wakisema kwamba watu
wapatao 50,000 walikuwa wakijaribu kuingia ndani ya uwanja huo.
0 Maoni