Timu ya taifa
ya Misri imetinga hatua ya Nusu fainali ya michano ya Afcon baada ya kufanya ‘come back’ ya kibabe dhidi
ya mahasimu wao wakubwa Morocco jana Januari 30, na kuibuka na ushindi wa magoli 2-1.
| Mohamed Salah akishangilia pamoaja na wachezaji wenzake baada ya Misri kutinga hatua ya nusu fainali ya Afcon. |
Morocco walikuwa
wa kwanza kutisa nyavu za Misri kupitia kwa Sofiane Boufal kwa mkwaju wa penati
dakika ya sita vao ambalo lilidumu mpaka mwisho dakika 5 zinamalizika.
Misri walianza
kulisakama lango la Morocco na kufanikiwa kusawazisha nahodha wao Mohamed Salah dakika 53.
| Mahamoud Trezeguet akishangilia baada ya kufunga goli la ushindi dhidi ya Morocco |
Baada ya dakika 90
za mchezo kuisha mechi ikiwa sare, zikaongezwa dakika 30 ambapo Mahmoud 'Trezeguet'
alifunga bao dakika ya 100 na kuipa uhakika Misri kutinga hatua ya Robo Fainali
Misri itacheza
na na wenyeji wa michuani hiyo Cameroon
Jumatano Februari 3, kwenye hatua nusu fainali ya kwanza, wakati nusu fainali
nyingine itakuwa kati ya Senegal dhidi ya Burkina Faso Jumanne Februari 2.
0 Maoni