Klabu ya soka ya Azam FC kupitia kwa Ofisa mtendaji mkuu Abdulkarim Amin leo Januari 25, imemtangaza Ahmid Moallin kuwa kocha mkuu wa kikosi hicho kwa maktaba wa miaka mitatu akirithi mikoba ya Mzambia George Lwandamina


Awali Moallin aliletwa kushika nafasi ya mkurugenzi wa ufundi wa maendeleo ya soka la vijana,  amefanikiwa kuifikisha Azam hatua ya fainali ya kombe la Mapinduzi ambao waliopoteza dhidi ya Simba.

 Kwenye ligi ya NBC ameanza vema akiingoza  Azam kushinda michezo miwilli ya ugenini dhidi ya Mbeya Kwanza 1-0 na Tanzania Prisons walioshinda kwa mabao 4-0.

Akizungumza mara baada ya kusaini kandarasi hiyo Moallin amesema Azam ni klabu kubwa huku akiamini kuwa anauwezo wa kufanya makubwa.

 "Azam FC ni klabu kubwa, na nililiona hili siku ya kwanza tu nilipofika hapa, nina amini katika klabu hii, nina amini katika uwezo wa klabu hii, klabu hii ina nafasi ya kufanya makubwa,"