Klabu ya Yanga imetangaza kuwa kiungo wao Raia Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Mukoko Tomombe anaondoka na kujiunga na Klabu ya TP Mazembe.
Aidha, Yanga hawajaweka wazi iwapo Mukoko kama ameenda kwa mkopo au ameuzwa jumla ila taarifa zilizopo alikuwa na mkataba wa miezi sita na Yanga.
Mukoko alijiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu wa 2020/2021 akitokea AS Vita ya Congo, lakini uwepo wa Khalid Aucho Yanick Bangala Gift Mauya na sasa ameongezeka Salum Abobakar 'Sure Boy' umefanya Mukoko kuwa chaguo la nne la kocha Nasreddine Nabi
0 Maoni