Klabu ya Yanga leo Januari 19, imecheza mchezo wa kirafiki
dhidi ya Mbuni Fc na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 mechi iliyochezwa kwenye uwaznja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha
Mabao ya Wananchi yamefungwa na Mukoko Tomombe 'Teacher' kwa njia ya mikwaju ya penati katika ya 56’ na 82
Yanga imetumia wachezaji wake wengi ambao hawapati nafasi ya kucheza na pia mashabiki wa Yanga walifanikiwa kumuona nyota
mpya Chiko Ushindi kwa mara ya kwanza akicheza ndani ya uzi wa Yanga.
Wananchi wapo Arusha wakijiandaa na mchezo wa ligi kuu ya NBC
dhidi ya Polisi Tanzania
0 Maoni