MABONDIA wawili wa Tanzania, Hassan Mwakinyo na Ibra Class, wamevuliwa mikanda ya ubingwa WBF Intercontinental na Shirikisho la ngumi za kulipwa la dunia la WBF.



Taarifa iliyotolewa na WBF imeeleza kuwa, mabondia hao sio mabingwa tena wa mikanda ya WBF kwenye uzani wa Super Welter (Kg 70) na Super Feather (Kg 59) ambayo walikuwa wakiishikilia Mwakinyo na Class hapo awali.




Imeelezwa kuwa sababu ya wawili hao kuvuliwa ubingwa huo, inatokana na wao kushindwa kuitetea mikanda hiyo kwa wakati husika kulingana na kanuni za WBF.



“WBF tumeumizwa na hiki kilichotokea, lakini kwa mujibu wa kanuni, hawa si mabingwa wetu tena baada ya kushindwa kutetea ubingwa kwao kwa wakati,”

Mwakinyo alitwaa ubingwa wa WBF Intercontinental baada ya kumchapa TKO ya raundi ya nne bondia Muargentina Jose Carlos Paz, Novemba mwaka 2020.