Mwamuzi wa Tanzania Frank Komba ni miongoni mwa waamuzi watakao chezesha mchezo wa kundi C wa michuano ya AFCON mchezo kati ya timu ya taifa ya Gabon dhidi ya Morocco, mchezo unaochezwa leo Saa 4:00 Usiku katika muendelezo wa michuano hii inayoendelea nchini Cameroon.



 

Franka Komba kwenye mchezo huu atachezesha kama mwamuzi msaidi namba 2, akimsaidia mwamuzi wa kati Dahane Beida kutoka Mauritanian mwamuzi msaidizi namba 1 ni Attia Amsaad kutoka Libya na mwamuzi wa akiba (fourth referee) ni Maguette Ndiay kutoka Senegal.


 

Komba ni mwamuzi pekee kutoka Tanzania aliyeorodheshwa na Shirikisho la soka barani Afrika CAF kuchezesha michuano hii ya mataifa barani Afrika.


 

Kabla ya kuanza kwa michuano hii Komba aliwahi kusema kuwa moja ya ndoto yake kwenye kazi ya uamuzi wa mpira wa miguu ilikuwa ni kuchezesha kwenye michuano hii mikubwa kwa ngazi ya timu za taifa barani Afrika.