Azam Fc wamefanikiwa kuitungua Namungo Fc kwa bao 1-0 ya
mkoani Lindi kwenye michano ya kombe la mapinduzi inayoendelea kutimua vumbi
visiwani Zanzibar.
Goli pekee la Azam limekwamishwa wavuni na Keneth Muguna
aliyefunga dakika ya 67, baada ya piga nikupige iliyotokea langoni mwa Namungo
FC na kuihakikishia timu hiyo kutinga hatua ya Nusu Fainali.
Muguna amechaguliwa kuwa mchezaji
bora wa mechi na kuondoka na kitita cha Tsh. 500,000 (laki tano)
michuano hiyo itaendaelea tena kesho mabingwa watetezi Yanga watacheza na KMKM saa 10:15 ba Simba dhidi ya Mlandege Fc majira ya saa 2:15 usiku
0 Maoni