Pamoja kuwa bora kwenye hatua ya makundi na kumaliza wakiongoza kundi lao kwa pointi 9 bila kupoteza mchezo, timu ya Taifa ya Nigeria imeambulia kichapo cha bao 1-0 kutoka wa Tunisia na kuondoshwa katika michuano ya Afcon 2021 nchezo uliochezwa jana usiku.
Bao pekee la Tunisia limefungwa na Youssef Msakni dakika ya 47 na kuwapeleka robo fainali ya michuano hiyo huku Alex Iwobi wa Nigeria akilamba kadi nyekundu dakika chache tu baada ya kuingia akitokea benchi.
Nigeria ambayo imeingia hatua ya robo fainali, ni mojawapo ya timu
ambazo zilikuwa zinapewa nafasi ya kuibuka na ubingwa kwenye michuano hiyo
unayoendelea Cameroon.
0 Maoni