Kinda wa Yanga, Denis
Nkane alisajiliwa hivi karibuni akitokea Biashara United atakuwa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja kutokana na
kusumbuliwa na Kinena.
Nkane alisajiliwa na Yanga kwenye dirisha dogo la usajili akitokea Biashara United, huku kwa sasa akiwa amecheza mechi mbili za michuano ya Mapinduzi.
Kiungo huyo
aliumia kwenye
mchezo wa hatua ya makundi
dhidi ya KMKM kwenye
Kombe la Mapinduzi.
Kwa
mijinu wa Gazeti la Championi , Daktari waYanga, Youssef Mohammed, alisema kuwa: “Kwa sasa kuna jumla ya wachezaji wanne ambao ni majeruhi kwenye kikosi.
“Denis
alipata majeraha kwenye mchezo wa mwisho wa makundi ambapo kwa sasa anasumbuliwa na Kinena, tatizo ambalo litamuweka nje kwa muda wa mwezi mmoja.”
0 Maoni