Kocha wa Mabingwa Afrika, Al Ahly ya Misri Pitso Mosimane (57) raia wa Afrika Kusini inaripotiwa kuwa anataka mshahara wa Dola za Marekani, 195,000 (Tsh milioni 450) kwa mwezi katika mpango wa kuongeza mkataba mpya Al Ahly, ikiwa ni ongezeko la USD 50,000 (Tsh Milioni 115) kutoka kwenye mshahara wake wa sasa.




Mkataba wake mpya anataka uwe na kipengele cha miezi 6 kupewa taarifa kabla ya kuvunja mkataba wake kutoka miezi mitatu iliyokuwa kwenye mkataba wa sasa.