Klabu ya Manchester United imempatia ofa ya mkataba mpya kiungo wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba wenye thamani paundi £500,000 kwa wiki na kumfanya nyota juyo kuwa Mchezaji anayelipwa fedha nyingi zaidi katika Ligi Kuu ya England (EPL)
Pogba anayeuguza majeraha anatarajia kurejea
Uwanjani Mwishoni mwa mwezi huu msimu huu wa mwaka 2021/2022 kiungo huyo ameichezea
Manchester Utd katika michezo 9 na Kutoa pasi "Assist" 7 zilizozaa mabao.
Mkataba wa Pogba unamalizika mwishoni mwa msimu
huu, ofa hiyo imekuja ikiwa ni siku chache baada ya united kumtambulisha afisa
mtendaji mkuu mpya Richard Arnold
anayetarajiwa kuanza majukumu yake mapema mwezi Februari.
0 Maoni