Manchester United wakiwa kwenye uwanja wa nyumbani Old Trafford wameondka na pointi tatu muhimu mbele ya West Ham United kwenye mchezo wa ligi kuu ya England

 



Goli la United limefungwa dakika za lala salama  90+3 na Marcus Rashford aliyeingia kipindi cha pili, akipokea pasi ya Edson Cavani.

 

Ushindi huu ulikuwa muhimu kwa United katika mbio zao za kusaka nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi ya Epl.


Leo United  kutoka nafasi za saba mpaka ya nne wakiwa na pointi 38 baada ya kushuka dimbani mara 22, wakiishusha West Ham ambao wamesalia na alama 37.