Klabu ya Simba leo Januari 14, 2022  imethibitisha kurejea kwa kiungo mshambuaji Clatous Chota Chama kwenye klabu hiyo.





 Chama amejiunga na Simba akitokea Rs Berkane ya Morocco kwa mkataba wa miaka miwili alijiunga na Simba mwaka 2018 na kuondoka mwaka 2021 kabla ya kurejea Simba na kutambulishwa rasmi leo ambapo bango kubwa lililotolewa na Simba likiwa na picha ya Chama linasomeka “Karibu nyumbani, Welcome home”


Chama aliondoka Simba SC Augusti 13 2021 na kujiunga  na RS Berkane ya Morocco na sasa anarejea baada ya kudaiwa kushindwa kuzoea mazingira nchini Morocco.