Klabu ya Everton ya nchini England,leo Januari 31,  imetambulisha rasmi Frank Lampard kuwa meneja wao, akirithi mikoba ya kocha  Rafa Benitez aliyetimuliwa hivi karibuni, staa  huyo wa  zamani wa Chelsea amepewa mkataba wa miaka wiwili na nusu kuionoa timu hiyo.

 



Lampard anarudi tena kwenye Premiere League baada ya kuingoza Chelsea tangu Julai 14, 2019 mpaka Januari 25, 2021, ambapo alitimuliwa na klabu hiyo kutokana na mfululizo wa matokeo yasiridhisha.