Real
Madrid imefanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya mahasimu wao
wakubwa Barcelona kwenye mchezo wa nusu fainali ya Spanish Super Cup uliochezwa
huko Saudi Arabia.
Madrid
walikuwa wa kwanza kutisa nayvu za Barca kupitia Vinicius Jr dakika ya 25, Luuk
de Jong alisawazishia Barca dakika ya 41 na kwenda mapumziko wakiwa sare ya bao 1-1.
Kipindi
cha pili Mfaransa Karim Benzema alikwamisha mpira ndani ya kimia na kuipa Los
Blancos uongozi dakika 72.
Vijana
wa Xavi walirejea na kusawazisha kupiti kwa Ansu Fati dakika ya 83' aliyesababisha mchezo kuongezwa dakika
30 (Extra Time) ili kumpata mshindi.
Aliyepeleka
kilio kwa Barca alikuwa Federico Valverde ambaye alifunga dakika ya 98' na kuipeleka
Reala Madrid Fainali ya Spanish Super Cup
Ikiwa
ni El Classico yake ya Kwanza kama kocha wa Barcelona Xavi Hernandez amekiri
kuwa kwa sasa wapinzani wao wamewacha mbali inabidi wafanye kazi ya ziada
kuwafikia Madrid walipo.
0 Maoni