Staa wa Manchester United, Cristiano Ronaldo hakufurahishwa
na uamuzi Kocha Ralf Rangnick baada ya
kumpumzisha dakika ya 70 nafai yake
kuchukuliwa na Harry Maguire kwenye ushindi wa mabao 3-1 mchezo wa ligi kuu dhidi ya Brentford.
Ronaldo alimuuliza Rangnick kwa nini aliamua kumtoa yeye na
sio mtu mwingine, akijibu swali la mwandishi baada ya mechi kuisha kocha huyo
wa muda wa United amesema alimwambia Ronaldo kuwa amefanya maamuzi hayo kwa
maslahi ya timu maana yeye ni meneja
"Wiki iliyopita mpaka dakika ya 70 tulikuwa mbele kwa magoli
mawili lakini baada ya filimbi ya mwisho matokeo yalikuwa 2-2 sikutaka hali ijirudie
tena" alisema Rangnick
0 Maoni