Kamati ya Uendeshaji na usimamizi wa Ligi ya Soka Tanzania Bara TPLB imempiga faini ya jumla ya Tsh milioni 3.5, Kocha Mkuu wa Simba SC, Pablo Martin Franco kutokana na makosa mbalimbali ya utovu wa nidhamu.




Pablo ametozwa faini ya Tsh 500,000 na kufungiwa mechi tatu kwa kosa la kupiga teke chombo cha kuhifadhia barafu na vinywaji (Mechi ya Simba vs Mtibwa Sugar).


Mhispania huyo faini ya Tsh. 1,000,000 kugomea mahojiano mechi dhidi ya Mtibwa Sugar.

Pia kamati hiyo imetoza faini ya Tsh. 1,000,000 kugomea mahojiano mechi dhidi ya Mbeya City.

Na mwisho imemtoza faini ya Tsh. 1,000,000 kwa mara nyingine kwa  kugomea mahojiano mechi dhidi ya Kagera Sugar