Waziri wa mambo ya Ndani wa Australia Karen Andrews amesema mcheza
Tenisi namba moja Novack Djokovic anaruhusiwa
kuondoka nchini humo muda wowote na hajashikiliwa kama ambavyo inaripotiwa vyombo
vya habari.
Djokovic 34 yupo karantini akisubiri rufaa aliyoikata kupinga
kufutiwa visa yake kwa, rufani hiyo itasikilizwa jumatatu.
Nchini Serbia kumekuwepo na maandamo kutoka kwa mashabiki
wakishinikiza kuachiwa huru kwa mshindi mara 20 wa Grand Slam.
Michuano ya Australian Open inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari
10 mpaka 30 mwaka huu.
0 Maoni