Staa wa Liverpool Mohamed Salah, jana amefanikiwa kuipa alama tatu Misri baada ya kufunga bao pekee dhidi ya Guinue-Bissau.

 


Salah amepachika goli kipindi cha pili dakika 69’ na kuwapa mafarao alama tatu za kwanza baada ya mechi ya kwanza kupoteza dhidi ya Nigeria.

 

Mchezo wa awali Nigeria iliitungua Sudan kwa mabao 3-1 na sasa imefikisha alama 6 ikiongoza kundi D, na kujiwekea mazingira mazuri ya kufuzu kwa hatua ya Robo Fainali, Misri wakiwa nafasi ya pili na alama 3 Guinea-Bissau na Sudan wana alama 1.