Staa
wa Liverpool Mohamed Salah, ameweka wazi kuwa suala ya yeye kuondoka au kubaki
kwa majogoo hao wa jiji lipo mikononi mwa klabu hiyo kwa sababu wanajua
anachotaka ili kuendelea kusalia kukipiga Anfeld.
Mkataba
wa Salah 29, unaisha mwakani 2023 huku wamiliki wa Liverpool wakihaha
kuhakikisha wanampa mkataba mpya.
“
Naijua klabu, nawapenda mashabiki Nataka kubaki lakini hili lipo nje ya mikono yangu
lipo chini yao kwa sababu uongozi
wanajua ninachotaka” amenukuliwa Salah.
Imeripotiwa
kuwa Salah anataka kulipwa Paundi 300,000 mpaka 350,000, sawa na Bil 1 na ushee za kitanzania, msimu huu tayari amefunga
magoli 23 kwenye michezo 26 aliyocheza.
Kwa
sasa Salah yupo nchini Cameroon a timu ya taifa ya Misri inayoshirikia michuano
ya Afcon
0 Maoni