Mohamed Salah ameipeleka Misri robo fainali ya michuano ya Afcon baada ya kupiga mkwaju wa penati wa mwisho baada dakika 120 kumalizika bila kumpata mshindi.



 Mlinzi wa Manchester United Eric Bailly alikosa mkwaju wa penati katika penati tano walizopiga Ivory Coast.

 

Misri iliibuka na ushindi wa penati 5-4, kwenye mchezo huo wa 16 bora, Misri sasa itakutana na Morocco kwenye hatua ya robo fainali.

 




Mechi myingine za robo fainali ni kati ya Cameroon dhidi ya Gambia, Burkina Faso watacheza na Tunisia, Senegal  watavaana Equtorial Guinea mechi hizo  zitachezwa Januari 29& 30.