OFISA Mtendaji Mkuu (CEO) wa klabu ya Yanga, Senzo Mbatha ameweka wazi kuwa kwa moto ambao kikosi chao kinaendelea kuuwasha kwenye Ligi Kuu Bara, wanaamini kuwa ni suala la muda tu kabla hawajatangazwa kushinda ubingwa msimu huu.



 

Akizungumzia mipango yao ya ubingwa msimu huu, Senzo alisema:“Tunajivunia mwenendo ambao kikosi chetu kimekuwa nao kwa michezo yote 13 ya kwanza, ni wazi tumefanya kazi kubwa kufikia hapa na binafsi kuona tunaweza kupata matokeo katika michezo migumu ugenini kama vile dhidi ya Coastal Union na Polisi Tanzania tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita.


“Hili linanionyesha wazi kuwa kwa kiasi kikubwa tuna nafasi kubwa ya kuibuka mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, nadhani ni suala la muda tu na tunapaswa kuendelea na kasi hii mpaka mwishonimwa msimu.”