Simba inajitupa uwanjani kucheza
na Mtibwa Sugar Leo Januari 22 ikiwa na
kumbukumbu ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Mbeya City kwa bao 1-0.
Timu hizo zinatarajiwa kuvaana
katika mchezo wa Ligi Kuu Bara leo Jumamosi saa kumi kamili kwenye Uwanja wa
Manungu, Morogoro.
Simba itawakosa kiungo Jonas Mkude na mshambuliji Kibu
Denis kutokana na majeraha, kwa upande wa Mtibwa Sugar Kocha Salum Mayanga amesema
anaamini Simba itakuja kivingine lakini wao wamejiandaa kushinda.
0 Maoni