Yanga
Princess leo, Januari 08, 2022 itawaalika mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya
Wanawake ya Serengeti Lite Simba Queens mchezo unaotarajiwa kupigwa saa 10:00 jioni katika
Dimba la Benjamin Mkapa, jijini Dar es
Salaam.
Katika mechi sita waliyokutana
Yanga Princess imefungwa michezo mitano huku ikiambulia sare kwenye mchezo
mmoja
Safu ya ushambuliaji ya Simba
Queens ni tishio kwenye ligi hiyo kwenye mechi tatu imefunga magoli 27 wakati
Yanga Princess imefunga magoli 6.
Haya ni matokeo ya mechi za
watani hao wa jadi walipokutana.
Yanga Princess 1-7 Simba Queens
Simba Queens 5-1 Yanga Princess
Simba Queens 3-0 Yanga Princess
Yanga Princess 1-3 Simba Queens
Simba Queens 0-0 Yanga Princess
Yanga Princess 0-3 Simba Queens
0 Maoni