SIMBA Queens imeendeleza rekodi ya ubabe mbele ya Yanga Princess
kwa kuendeleza vipigo kwenye msimu wao wa nne mfululizo baada ya kuibuka na
ushindi wa mabao 4-1 katika mchezo uliopigwa jana Uwanja wa Mkapa Dar es salaam.
Simba Queens imeweka rekodi ya kushinda mechi sita kati ya saba
ilizowahi kukutana na Yanga kwenye ligi.
Ushindi huo umeifanya Simba kurudi kileleni kwenye msimamo wa
ligi na kuishusha Fountain Gate ambayo ilikuwa inaongoza kwa alama tisa wakati
Simba baada ya kushinda imekusanya alama 11.
Mabao ya Simba yalifungwa na Oppah Clement aliyefunga mawili
pamoja na Asha Djafar ambaye pia alifunga mawili huku bao pekee Yanga
likufungwa na Aisha Masaka kwa mkwaju wa penalti.
0 Maoni