Uongozi wa klabu ya Simba umethibitisha kuachana na wachezaji wake watatu katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili kwa makubaliano ya pande zote huku mmoja akitolewa kwa mkopo.
Wachezaji ambao walio ondolewa kwa makubaliano ni Duncan Nyoni na AbdulSamad Kassim huku mlinda mlango Jeremiah Kisubi akijiunga na Mtibwa Sugar kwa mkopo hadi mwisho wa msimu.
Wachezaji hao wanafanya idadi ya walioondoka kwa makubaliano na klabu ya Simba kuwa watatu baada ya Ibrahim Ajibu kujiunga na Azam FC wiki iliyopita.
0 Maoni