Timu ya  Simba imefanikiwa kuanza vyema michuano ya kombe la Mapinduzi  na kunjinyakulia alama tatu, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao  2- 0 dhidi ya Selem View  mchezo ulichezwa kwenye dimba la Aman, Zanzibar.







Magoli ya Simba yamepachikwa na Pape Osmane Sakho ambaye yupo kwenye kiwango bora kunako dakika ya 25 na kwenda mapumnziko wakiwa kifua mbele kwa bao 1-0.


Kipindi cha pili Simba iliongeza bao la pili kwa mkwaju mkali nje ya 18, uliopigwa na Kiungo fundi raia wa Zambia Larry Bwalya.