Bingwa mtetezi wa ligi kuu ya NBC Simba leo Januari 22, imeshindwa kufua dafu mbele ya Mtibwa Sugar, mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Manungu Turiani Mkoani Morogoro.

 


Mazingira ya uwanja  leo hayakuwa rafiki kutokana na kuwa na maji na tope baada ya mvua kunyesha, timu zilijaribu kutafuta nafasi za kufunga  lakini maji yalipunguza ladha ya soka ambalo timu zote zingeweza kuonyesha.

 

Mwamba wa Lusaka, Clatous Chama alicheza mechi ya kwanza tangu arejee kwenye Simba na kuingia kwake kulibadilisha mchezo kwa Simba na kuanza kufika mara kwa mara kwenye lango la Mtibwa Sugar.

 


Simba sasa inafikisha alama 25 baada ya kucheza michezo 12 na mahasimu wao Yanga wanaendelea kubaki kileleni na alama 32, na kesho  itashuka dimbani dhidi ya Polisi Tanzania