Simba baada ya kushindwa kufunga goli kwenye michezo mitatu ya ligi, Jana usiku imetoa dozi nzito ya magoli 6-0 kwa timu ya Dar City kwenye mchezo wa hatua ya 32 wa Azam Sports Federation Cup (ASFC) uliopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa Dar es salaam.
Mashabiki wakiwa na
shauku kubwa ya kumuona staa wao
aliyerejea Msimbazi Clatous Chama kwa mara ya kwanza kwenye dimba la Mkapa,
Simba walianza kuonyesha kuwa wamedhamiria kuondoka na ushindi baada ya
kufungua akaunti ya magoli kupitia kwa
Meddie Kagere aliyefunga magoli mawili katika dakika ya 5 na 13.
Tripple C alikwamisha vao
la tatu kwa Faulo matata dakika ya 18, na kisha ku asisti bao la Rally Bwalya dakika
ya 22 na kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 4-0.
Kipindi cha pili Pachal
Wawa akiwa na dakika mbili tu tangu ameingia dimbani, alikwamisha bao la tano dakika
ya 47 na Chris Mugalu akafunga karamu hiyo kwa kuweka wavuni bao la sita dakika
ya 80.
Simba sasa itavaana na Ruvu
Shooting katika hatua ya 16 bora
•Ruvu Shooting v Simba
•Yanga v Biashara United
•Pamba v Dodoma Jiji
•Tanzania Prisons v Polisi Tanzania
•Coastal Union v Mtibwa Sugar
•Kagera Sugar v Namungo
•Baga Friends v Azam FC
•Mbuni/Lipuli v Geita Gold
0 Maoni