Mabingwa wa ligi kuu Tanzania  bara Simba  leo Januari 3, imezindua jezi mpya  ambazo watazitumia katika michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) na Mapinduzi Cup ambayo imeanza kutimua vumbi visiwani Zanzibar.

Simba tayari imewasili visiwani humo kwa ajili ya michuano hiyo ambapo Januari 5m itashuka dimbani kuvaana na Selem View saa 10:00 jioni.