Timu
ya Simba leo Januari 13, imefanikiwa kutwaa ubingwa w kombe la mapinduzi baada ya kuicha Azam
Fc kwa bao 1-0 mchezo uliochezwa uwanja wa Amaan, Zanzibar
Goli
pekee la Simba limefungwa na mshambuliaji Meddie Kagere dakika ya 56’ kwa
mkwaju wa penati baaya mlinda mlango wa Azam Fc KIgonya kumfanyia faulu Pape
Osmane Sakho.
Kwa
ushindi huo mnyama Simba amemaliza uteja mbele ya Azam Fc baada ya kupoteza
fainali tatu za kombe la mapinduzi.
Mlinda
mlango wa Simba Aishi Manula amechaguliwa kuwa Golikipa bora wa michuano hiyo
akiwa hajafungwa bao, Pape Sakho amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mashindano
hayo na Fowadi Meddie Kagere akiwa ndiye mfungaji Bora.
Mchezaji
wa bora fainali amechaguliwa beki mkongomani Inonga Baka
0 Maoni