Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania TFF leo Januari 24, limekanusha kumfungulia kesi Polisi kiongozi yoyote wa mpira wa miguu.
Shirikisho hilo linawataka wanaondesha propaganda
hizo kuacha mara moja, kwani hawatasita
kuchukua hatua stahiki kwa wote wanaoendelea kusamabaza.
Mapema siku ya leo kumeibuka taarifa zilizokuwa zikidai Shirikisho hilo limemfungulia Mashtaka Barbara Gonzalez kwa kitendo cha kutoa lugha Chafu wakati wa mchezo wa Simba na Yanga Disemba 11 mwaka jana, baada ya kuzuiliwa kuingia eneo la VVIP na watoto ambao kiutaratibu hawaruhusiwi.
0 Maoni