Mlinzi wa kulia wa Timu ya Taifa ya England Kieran Trippier
amejiunga na Newcastle United kwa mkataba wa miaka miwili na nusu.
Trippier ambaye alikuwa akikipiga Atletico Madrid ya Hispania amsajiliwa
kwa paundi mil. 12 amekuwa mchezaji wa
kwanza kusajiliwa na matajiri wa Saudia Arabia ambao ni wamiliki wapya wa klabu
hiyo.
Mchezaji huyo wa zamani wa Spurs ametumia ukurasa wale kwenye mtandao
wa Instagram kuonyesha furaha yake baada ya ukamilisho huo kukamilika.
Ninafuraha kujiunga na Newcastle kila mtu anajua mashabiki wake ni
wakipeee nasubiri kwa hamu kuanza mazoezi na wachezaji wenzangu, na kuingia
kucheza kwenye uwanja wa St. James Park.
0 Maoni