Unaweza kuwa mwanzo mbaya kwa kwa vigogo wa soka Afrika Kaskazini kwenye michuano ya Afcon inayoendela nchini Cameroon, baada ya
Misri kupoteza dhidi ya Nigeria, Algeria kulazimishwa Sierra Leone sare, leo Tunisia imeangukia pua baada ya
kufungwa na Mali kwa bao 1-0 mchezo wa kundi F
Goli pekee la Mali limekwamishwa wavuni na Ibrahima Kone dakikia ya 49 kwa mkwaju wa penati baada ya
beki wa Tunisia kuunawa mpira ndani ya 18.
Nahodha wa Tunisia Wahbi Khazri alikosa mkwaju wa penati dakika
ya 77 baada ya mlinda mlango wa Mali Mounkoro
kupangua mkwaju huo.
El Bilal Toure alilimwa kadi nyekundu dakika ya 87, na
kuwifanya Mali kucheza Pungufu uwanjani, mwamuzi aliingia kwenye mzozo na
benchi la ufundi la Tunisia wakiadai alimaliza mchezo kabla ya muda.
0 Maoni