Bodi ya Ligi kuu Tanzania TPLB imeufungulia uwanja wa Manungu  uliopo Turiani mkoani Morogoro kuendelea kutumika kwa michezo ya ligi, hatua hiyo imekuja baada ya kufanyiwa ukaguzi na kuthibitika unakidhi vigezo vya kikanuni.

 





Uwanja huo ulifungiwa baada ya eneo la kucheza (pitch) ulikosa sifa za kikanuni kufuatia taarifa hiyo mchezo wa ligi ya NBC namba 102 kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Simba uliopangwa kuchezwa uwanja wa Jamhuri Morogoro sasa utachezwa kwenye uwanjan wa Manungu.